Uzinduzi wa Ubalozi mdogo wa Mauritius jijini Dar es Salaam,Tanzania tarehe 3 Agosti, 2017 uliofanyika katika ofisi za ubalozi huo na mgeni rasmi akiwa Waziri wa Biashara na Masoko wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar , Balozi Amina Salum Ali . Ubalozi huu utafungua fursa kwa watanzania katika kuendeleza uchumi wa Nchi , kufungua njia kwa wawekezaji wa Nchi hiyo kuwekeza katika sekta ya sukari nchini Tanzania ambapo ofisi hii pia itakua chanzo na fursa ya kupanua wigo la uwekezaji katika sekta zengine kama Uvuvi, Kilimo na Utalii . Aidha Mh Amina Salum Ali ametilia mkazo katika uwekezaji kwenye sekta ya sukari na kuendeleza viwanda kama athma ya Serikali awamu ya tano ikiwa ni msingi wa Maendeleo.
No comments:
Post a Comment